Thursday, May 11, 2017

Mugabe huwa anapumzisha macho si kulala

Bw Mugabe akiwa mkutanoni Afrika Kusini wiki iliyopita
Bw Mugabe akiwa mkutanoni Afrika Kusini wiki iliyopita
 
Msemaji wa Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe amesema kiongozi huyo huwa anapumzisha macho tu na si kulala wakati wa mikutano kama wanavyoamini watu wengi.
Kiongozi huyo amekuwa akionekana kusinzia katika mikutano mingi.
"Rais huwa anasumbuliwa na mwanga mkali," George Charamba amenukuliwa akisema na gazeti la serikali la Herald.
Rais huyo kwa sasa yupo nchini Singapore akipokea matibabu maalum kwenye macho yake.
Bw Mugabe, 93, anapanga kuwania tena urais katika uchaguzi mkuu mwaka ujao.
"Huwa najihisi kama mtu ambaye amekosa kutekeleza kazi yake vyema ninaposoma (kwenye vyombo vya habari na mtandaoni) kwamba rais alikuwa anasinzia katika makongamano - la hasha," Bw Charamba amesema.
Alilinganisha tatizo la Bw Mugabe na matatizo ya macho ambayo yalikuwa yanamsibu Rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela.
Bw Mandela alikuwa anatatizwa na mwanga mkali na wapiga picha hawakuruhusiwa kutumia mwanga wa kamera wakati wanapiga picha katika hafla zake.
Matatizo ya Bw Mandela yalitokana na kufanya kazi kwa muda mrefu katika timbo na pia kufungwa jela muda mrefu Robben Island.
Mugabe Bamako Januari 13, 2017.
Macho ya Robert Mugabe hutatizwa na mwanga, msemaji wake amesema. Hapa Mugabe anaonekana akiwa Bamako Januari 13, 2017.
Safari za Bw Mugabe za mara kwa mara nje ya nchi zimekuwa zikishutumiwa sana na wakosoaji wake.
Sekta ya afya nchini Zimbabwe imedorora na wahudumu wa afya hulalamika kwamba huwa hawalipwi vyema.

No comments:

Post a Comment

Trump: Sichunguzwi na FBI

Rais Trump anasema kuwa hachunguzwi   Rais wa Marekani Donald Trump amesisitiza kwa...