Shule zote katika kisiwa cha Zanzibar zimefungwa kwa muda kutokana na mvua kali ambayo imesababisha mafuriko.
Waziri
wa elimu katika kiswa hicho Riziki Pembe Juma amesema kuwa mvua hiyo
ambayo pia imekuwa ikinyesha katika kisiwa cha Unguja na Pemba kwa
kipindi cha wiki tatu zilizopita pia imeharibu barabara na mali ya watu.Alisema kuwa baadhi ya shule zimejaa maji hivyobasi kuwa vigumu kwa walimu kufunza mbali na kuwa wanafunzi wanashindwa kufika kutokana na mafuriko.
- Watu 250 waangamia kwenye maporomoko ya ardhi Colombia
- Utalii Tanzania wazidi kuimarika
- Virusi vya Zika vyapatikana Tanzania
Baada ya kuangazia mapendekezo hayo tulikuwa hatuna njia nyengine bali kuzifunga shule hadi pale hali itakaporudia hali yake ya kawaida.
Hatahivyo amesema kuwa wanafunzi wa kidato cha sita waliokuwa wakifanya mitihani yao ya mwisho wataendelea kufanya hivyo.
Kufikia sasa kuna takriban wanafunzi 364 495 wa shule za msingi na zile za upili zanzibar.
Source:BBCSwahili
No comments:
Post a Comment