|
Muigizaji wa filamu za Bongo Elizabeth Michael ‘Lulu’. |
MAYASA MARIWATA | AMANI | MAKALA
KUTOKANA na wasanii wa fi lamu za Kibongo
kuwa kwenye mikakati mizito ya kuhakikisha soko la kazi zao linarejea
kwenye ubora wake kwa madai kuwa filamu za nje zimeua soko la ndani,
kuna haja ya kuyazingatia haya yanayochangia kufeli kwao ili kupaa na
kufi kia levo ya kimataifa.
Muigizaji wa Filamu, Kajala Masanja.
- UBORA WA STORI
Ninapozungumzia ubora wa stori moja kwa moja nawalenga waandishi wa
script, unakuta mtu unaamua kuangalia filamu kwa bashasha ukiamini
‘utainjoi’ lakini mambo yanakuwa tofauti, unaitabiri fi lamu mwanzo
mwisho na kweli itaenda hivyo.
Mfano unaweza ukasema hapo si kamsaidia lazima atamtongoza na kweli
itakuwa hivyo, hapo ataingia chumbani kujifi cha basi itakuwa hivyo,
unaweza ukakuta fi lamu nzima itaenda vile unavyohisi utadhani wewe
ndiyo umeiandika, tofauti kidogo na fi lamu za wenzetu wanajitahidi
kucheza na akili ya kawaida ya binadamu.
- KURUDIA STORI
Kuna stori ambazo zimerudiwa `idea’ aidha kwa msanii mmoja au wasanii
tofauti kuiga kazi ya mwenzao, mfano kuna fi lamu ya kaka mkubwa
Vincent Kigosi `Ray’ aliicheza miaka ya nyuma, yeye ni mtoto wa tajiri
lakini aliamua kuishi kimaskini na kwenda kufanya kazi kwenye nyumba ya
matajiri kisha mtoto wa bosi akampenda.
Cha kustaajabisha siku chache zilizopita katoa fi lamu ya kufanana na
hiyo ya Geat Keeper na yenyewe, Ray baba yake ni tajiri lakini yeye
kaamua kuishi kimaskini na kwenda kufanya kazi nyumba ya matajiri na
mwisho motto wa bosi akampenda na kuwa naye, swala hili pia linapunguza
mvuto kwa mashabiki.
- KUJUANA
Kuna tabia ambayo inafanywa na wasanii wengi ambayo hata baadhi yao
wamekuwa wakilalamikia jambo hilo kuua soko, yaani msanii anavutiwa na
muonekano wa mtu f’lani na kuamua kumchezesha kwenye fi lamu yake bila
kumfanyisha mazoezi zaidi ya kumpa script aisome basi, matokeo yake
anajikuta ‘akimbwela’ kwenye kamera na kuwafanya hata watazamaji
wamshtukie na kuchukizwa naye.
- MAMBO YA KIZUNGU
Jambo hili linawahusu sana upande wa akina dada, unatazama fi lamu
unaandikiwa miaka mitatu nyuma au mbele lakini cha kushangaza nywele ni
zilezile zikiwa kwenye msuko uleule tena nywele za bandia, rasta au
wigi, wakati nywele hizo haziwezi kusukwa miaka mitatu bila kufumuliwa,
ina maana ni uongo wa wazi, pia usiku mtu kalala lakini kajazwa ‘make
up’ si sawa.
- KUENDEKEZA UFUSKA
Muda mwingine ubora wa kazi unatoweka kutokana na tabia ya kuendekeza
ufuska ‘ngono’ mida ya kazi, wasanii wengi wanapenda kukaa kambini
lakini wakifika huko baada ya kuwaza kazi wanawaza mapenzi, hapo
utasikia f’lani katoka na f’lani, huyu kamuibia mpenzi yule, basi balaa
juu ya balaa matokeo yake muda wa kazi ukifi ka watu wanafanya ilimradi
tu siyo kwa kiwango kile walichokikusudia.
- WIVU WA MAENDELEO
Inapotokea msanii kawa juu kuliko mwingine baada ya kuungana na
mwenzao ili aweze kufanya vyema zaidi, wanaanza kumjengea chuki na
kufanya njama za kumdidimiza, kama wasanii wakongwe kuna msanii anaibuka
kwa kishindo basi mpeni sapoti ili afike mbali zaidi huenda akawavuta
na nyinyi mkatoboa kupitia yeye.
- UNAFIKI
Kitendo ambacho naweza kusema kinairudisha nyuma tasnia kwa kiasi
kikubwa ni hiki, baadhi ya wasanii wanawaza kufi tinishana muda wote
yaani hiyo ni moja ya starehe kwao, mtu akiona f’lani na f’lani
wanaelewana anawaza kuwachonganisha au wamekaa wanaongea vizuri mmoja
akiinuka tayari mwingine anampiga majungu yaani upendo wa kweli ziro.
- USTAA
Kufanya kazi kwa kujiona ni mastaa f’lani kama vile Jacqueline
Wolper, Wema Sepetu, Aunt Ezekiel, Jacob Steven ‘JB’, Chuchu Hans, Daudi
Michael `Duma’ na wengine hii inachangia kupoteza ubora, sababu baada
ya kuwa makini na unachokifanya unawaza tu mimi ni staa f’lani
nitatazamwa tu, kazi yangu itauzika tu, siku hizi watu wameeilimika
hawajali ustaa wa mtu wanachojali ni ubora wa kazi.
- KUTHUBUTU NA KUJIAMINI
Hili ni jambo la mwisho na la muhimu sana katika kuipeperusha vyema
bendera ya nchi yetu, ondokaneni na nidhamu ya uoga changamkeni kutafuta
chaneli ya kufanya kazi na wasanii wa nchi mbalimbali, ili kukuza soko
letu na kuzidi kuipa sifa nchi yetu, tukaondokana na ile dhana kwamba fi
lamu za Nigeria zinapendwa zaidi au za Kihindi au za Kizungu, kwa nini
isiwe za Kibongo?
Source:
GlobaPublishersTZ